Atabatu Abbasiyya imeandaa shindano maalum katika kuadhimisha mazazi ya Imamu Zainul-Aabidina (a.s).

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umeandaa shindano maalum katika kuadhimisha mazazi ya Imamu Zainul-Aabidina (a.s).

Majina ya washindi kumi wa mwanzo yatatangazwa siku ya Jumatatu jioni (19/02/2024m) saa kumi jioni kwenye jukwaa la Atabatu Abbasiyya tukufu.

Sharti la kupokea zawadi, mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Ali-Akbaru (a.s), itakayofanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) siku ya Jumatano (20/02/2024m) sawa na (10 Shabani 1445h) saa nane na nusu mchana.

Iwapo mshindi atapata udhuru wa kushindwa kuhudhuria kwenye hafla hiyo, atatakiwa Kwenda kwenye idara ya wahasibu katika Atabatu Abbasiyya ndani ya siku nne toka kutangazwa kwa majina hayo, akiwa na kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: