Majmaa-Ilmi imehitimisha msimu wa saba wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imehitimisha msimu wa saba katika mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa.

Mradi huo unasimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.

Mkuu wa kamati tendaji ya mradi huo Sayyid Muhammad Ridhwa Zubaidi amesema “Majmaa imehitimisha ratiba ya msimu wa saba katika mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, kwa kufanya shindano kwa wanafunzi walioshiriki katika mradi (Shindano la maasumina 14), lengo la shindano hilo ni kujenga uwelewa kuhusu Maisha ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Mradi ulikuwa na vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na utoaji wa mihadhara ya kitamaduni, kidini na kimaadili, bila kusahau masomo ya kila siku ya hukumu za usomaji wa Qur’ani, kwa kuzingatia mfumo wa usomaji wa Qur’ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: