Watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wamefanya tukio la kiibada ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abufadhil Abbasi (a.s) katika kuadhimisha kuzaliwa kwake.
Kiongozi wa idara ya kupokea wageni katika Ataba tukufu Sayyid Faarisi Husseini amesema “Watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wameadhimisha mazazi ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mbele ya kaburi lake takatifu, Pamoja na viongozi wa Ataba, wageni wa kongamano la kimataifa Rabii-Shahada awamu ya kumi na saba na kundi kubwa la mazuwaru waliokuja kuadhimisha tukio hili”.
Akaongeza kuwa, “Tukio limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na kisomo cha ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kisha wimbo wa (Lahnul-Ibaa), zikafuata qaswida na tenzi zilizotaja mazazi hayo matukufu, wakahitimisha kwa kugawa mauwa na pipi kwa mazuwaru”.
Rais wa ofisi ya Vatikan huko Roma ambae ni mmoja wa wageni wa kongamano, Muheshimiwa Matraan Dazani amesema kuwa, amefurahi sana kuhudhuria maadhimisho ya kuzaliwa miezi ya Muhammadiyya, Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na Imamu Zainul-Aabidina (a.s), akabainisha kuwa “Mazingira ya kiibada yaliyopo katika mji wa Karbala ni kielelezo cha upole, mshikamano na umoja katika jamii”.