Atabatu Abbasiyya tukufu imehitimisha hafla ya kuadhimisha kuzaliwa miezi ya Muhammadiyya, Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na Imamu Sajjaad (a.s).
Hafla imefanywa kwenye uwanja wa mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami, viongozi wengine wa Ataba tukufu, marais wa vitengo na watumishi wao pamoja na wageni waliowakilisha taasisi tofauti na kundi kubwa la mazuwaru.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyosomwa na msomaji wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Liith Ubaidi, ikafuatiwa na ujumbe kutoka uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, uliowasilishwa na Sayyid Adnani Jalukhani kutoka kitengo cha Dini.
Hafla imepambwa na qaswida, mashairi na tenzi zilizotaja mazazi hayo matukufu kutoka kwa Sayyid Nadhiri Mudhwafar, Zainul-Aabidina Saidi, Hassein Abuu Iraq na Ali Basha Karbalai.