Chuo kikuu cha Alkafeel kimekamilisha maandalizi ya kongamano la kimataifa awamu ya tano katika mkoa wa Najafu.
Chuo kitafanya kongamano la kimataifa awamu ya tano, litakalojikita katika fani za udaktari, uhandisi na elimu ya pesa tarehe (17 – 18) mwezi huu, kwa kushirikiana na hospitali ya rufaa Alkafeel pamoja na chuo kikuu cha Al-Ameed na Tolonto cha nchini Marekani.
Kamati ya wahandisi na mawasiliano zimekamilisha maandalizi yote ya kongamano hilo chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kongamano ni sehemu ya malengo ya chuo katika kiwango cha elimu, linasaidia kujenga ushirikiano na kuangalia tafiti za kielimu katika nyanja tofauti.