Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla kubwa katika kuadhimisha kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya katika ukanda wa kijani upande wa kusini.
Rais wa kitengo cha ukanda wa kijani upande wa kusini Sayyid Nasoro Hussein Mut’ibu amesema “Ataba tukufu inaendelea kufanya hafla za kuadhimisha kuzaliwa kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) katika maeneo tofauti, likiwemo eneo la ukanda wa kijani kibichi, imefanywa hafla kubwa iliyohudhuriwa na familia nyingi za raia wa Iraq katika siku ya pili”.
Akaongeza kuwa “Hafla hizi zinafanywa chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya kwa lengo la kutakasa nafsi na kuingiza furaha sambamba na kujenga uelewa wa Dini”.
Kiongozi mkuu wa jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo cha Habari na utamaduni Sayyid Ali Hussein amesema “Jumuiya inashiriki kwenye hafla zinazoandaliwa na Atabatu Abbasiyya kupitia vipengele vingi, kufanya maigizo, kuimba qaswida, kusoma Qur’ani Pamoja na vipengele elekezi na vinginevyo vinavyolenga kuelekeza jamii katika kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s)”.