Jumuiya ya Al-Ameed ya kielimu, imefanya kikao cha wajumbe wa kamati kuu.
Rais wa jumuiya Dokta Riyaadh Twaariq Ameedi amesema “Kikao kinahusu kamati kuu za jumuiya za kielimu, hufanywa mwezi wa pili kila mwaka chini ya maelekezo ya wizara ya elimu na tafiti za kielimu”.
Akaongeza kuwa “Kikao hicho ni nafasi ya kutaja mikakati na ratiba za jumuiya mbele ya wajumbe wa kamati kuu, sambamba na kuangalia bajeti hitajika na kuwakilishwa kwa wizara pamoja na kuangalia namna bora ya uboreshaji wa jumuiya”.
Kwa mujibu wa maelezo ya Ameedi, jumuiya ya Al-Ameed mwaka jana ilipata kitabu cha kupongeza mafanikio yake.