Kwa kugawa pipi na mauwa.. jumuiya ya Skaut ya Alkafeel imeadhimisha kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya.

Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeadhimisha kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya kwa kugawa pipi na mauwaa katika maeneo tofauti hapa mjini.

Tukio hili hufanywa katika tarehe za kuzaliwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) kwa njia tofauti, katika maadhimisho haya ya kuzaliwa miezi ya Muhammadiyya Imamu Hussein, ndugu yake Abulfadhil Abbasi na Imamu Sajjaad (a.s) wamegawa pipi na mauwa kwa mazuwaru wa mji mtukufu wa Karbala.

Vijana wa Skaut wamewekwa katika vikundi na kusambazwa kwenye Barabara za mkoa wa Karbala na katika mageti ya ukaguzi na malango makuu ya mji, kwa ajili ya kupokea watu wanaoingia katika mji huu mtukufu.

Maadhimisho ya kuzaliwa miezi ya Muhammadiyya ni nafasi ya kukuza uhusiano na Ahlulbait (a.s), sambamba na kuijenga jumuiya katika misingi ya ubinaadamu na uislamu.

Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel huandaa mamia ya ratiba za Skaut kwa mwaka, kwa lengo la kukuza nidhamu ya kufanya kazi kwa pamoja na kujenga ushirikiano na jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: