Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha ratiba ya kongamano la maadhimisho ya kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya katika mkoa wa Karbala mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa Karbala na mazuwaru.
Kongamano lilisimamiwa na jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kwenye moja ya viwanja vya ukanda wa kijani, katika kuadhimisha mazazi ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na Imamu Sajjaad (a.s) ndani ya mwezi huu wa Shabani.
Kongamano lilikuwa na vipengele vingi, kulikuwa na vituo vya usoamji wa Qur’ani, uchoraji, michezo ya wanaskaut, mambo ya kitamaduni, igizo lenye anuani isemayo (Kurudisha mtazamo), mazungumzo yenye anuani isemayo (Miwani ya ajabu), na mambo mengine mengi yaliyopata muitikio mkubwa kutoka kwa familia za wakazi wa Karbala.
Atabatu Abbasiyya huhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s) likiwemo hili la mazazi matukufu katika mwezi wa Shabani, kwa kufanya ratiba za kitamaduni na kidini.