Ameyasema hayo alipokutana na ugeni kutoka taasisi ya Aalil-Bait (a.s) ya Qur’ani tukufu katika mji wa Qum chini ya usimamizi wa Marjaa mkuu wa Najafu, ugeni huo umetoa maelezo kuhusu kazi za taasisi na nafasi yake katika kusambaza utamaduni wa kusoma Qur’ani, pia Muheshimiwa Sayyid Swafi amesikiliza usomaji wa Qur’ani kutoka kwa wajumbe wa ugeni huo, waliosoma maqamaat tofauti na mmoja wao akasoma kwa kuhifadhi.
Sayyid Swafi akabainisha kuwa, Qur’ani tukufu ni maneno ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, tunatakiwa kunufaika nayo, kila mwanaadamu atakavyo jitenga nayo ndivyo atakavyo potea.
Akaendelea kusema kuwa, katika Qur’ani tukufu kunanukta muhimu sana, ambazo ni vigumu kuzidiriki na kuzitafsiri zimebeba mambo tofauti, nazo zinaonyesha ukuu wa kitabu hiki, akasema; lugha ya kiarabu na ufasaha (balagha) vimefungamana na Qur’ani tukufu, kutenganisha lugha na balagha ni sababu ya kutoelewa maana nyingi ambazo huchukuliwa ni miongoni mwa siri za lugha ya kiarabu.
Akasisitiza kuwa, Maimamu wa Ahlulbait (a.s) waliijali sana Qur’ani tukufu, wameeleza mambo mbalimbali kuhusu usomaji wa Aya za Qur’ani na tafsiri zake, ukizingatia kuwa wao ndio wenye elimu na uelewa mkubwa wa kitabu hicho, miongoni mwa usia muhimu wa Mtume (s.a.w.w) unasema “Shikamaneni na vizito viwili Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu”, kwa hiyo tunatakiwa kufuata riwaya za Ahlulbait (a.s).
Akahimiza kuwa “Mnatakiwa kuliwazika na riwaya za Ahlulbait (a.s) wakati mnapozisoma kama mnavyoliwazika na Qur’ani tukufu, aidha tunatakiwa kudumu na kusoma dua zilizopokewa kutoka kwao (a.s), Nahjul-Balagha, Swahifatu-Sajaadiyya na vinginevyo”.
Sayyid Swafi akahusia kufanya mazingatio katika usomaji wa Qur’ani na sio kutosheka na kusoma tu, kufanya mazingatio kunaongeza mafungamano na Qur’ani na kujenga ukaribu na Mwenyezi Mungu (s.w.t), jambo hilo hukomaza akili na kukuwezesha kuona mambo kwa usahihi.
Akasema kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inaipa Qur’ani umuhimu mkubwa, imeanzisha idara maalum inayohusika na Qur’ani tu kwa jina la (Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu), imefanikiwa kutoa maelfu ya wahitimu wa Qur’ani wenye uwezo mkubwa katika sekta hiyo.
Haafidh wa Qur’ani tukufu na mkuu wa taasisi ya Aalil-Bait (a.s) Sayyid Muhammad Ali Islami amesema “Kikao chetu na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, kinafaida kubwa, amutuonyesha umuhimu wa kufundisha Qur’ani tukufu na namna Atabatu Abbasiyya inavyojali masomo ya Qur’ani”.
Akaongeza kuwa, Tumempa Muheshimiwa Sayyid Swafi ripoti kamili kuhusu ratiba ya taasisi inayohusisha mahafidh (60), wengi wao ni wasomaji wa kimataifa, ambao kwa sasa ni mabalozi wa Qur’ani katika nchi tofauti, akasema kuwa (30) katika hao wamejikita katika hifdhu ya Qur’ani.