Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya hafla kubwa ya kuadhimisha kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya katika jiji la Baghdad.
Hafla hiyo imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Baghdad chini ya Majmaa, kwa kushirikiana na taasisi ya Imamu Mahadi (a.f) katika Husseiniyya ya Sadrah kitongoji ya Raswafah.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Hassan Shaakir, kisha ikasomwa surat Faat-hah kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu, halafu akafuata msomaji wa Maahadi Husseini Alghazi, kisha akasoma Sajaad Maliki.
Hafla imepambwa na mashairi kutoka kwa Ali Dhahabi kuhusu tukio hilo tukufu.