Atabatu Abbasiyya imeshiriki katika ratiba ya mkutano wa wanawake katika kongamano la Rabiu-Shahada awamu ya kumi na saba.

Atabatu Abbasiyya imeshiriki kwenye ratiba ya mkutano wa wanawake katika kongamano la kimataifa Rabiu-Shahada awamu ya kumi na saba.

Atabatu Husseiniyya tukufu imefanya kongamano la kumi na saba kuanzia tarehe (3 – 7) ya mwezi wa Shabani, katika mnasaba wa kuadhimisha kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya.

Kiongozi wa idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya bibi Bushra kinani amesema “Tunapata msaada endelevu kutoka Atabatu Abbasiyya kutokana na mtazamo wa Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi kila anapoongea na wanawake, husema (Mwanamke ni tunu, nae anauwezo wa kujenga misingi ya utukufu na maadili mema, hivyo anatakiwa kuwa mwanamke imara)”.

Akaongeza kuwa “Idara ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya inamajukumu mengi, inakazi ya kumtambulisha bibi Zainabu (a.s) na nafasi yake katika harakati ya Imamu Hussein (a.s) sambamba na kuelekeza wanawake namna ya kupambana na vingozi waovu”.

Akasisitiza kuwa “Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya katika kongamano ni sehemu ya kuangalia kinachoweza kufanywa na Ataba tukufu katika kongamano la kimataifa Rabiu-Shahada”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: