Chuo kikuu cha Al-Ameed kimehuisha kumbukumbu ya kuzaliwa miezi ya Shaabaniyya.

Kitivo cha malezi katika chuo kikuu cha Al-Ameed kimefanya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa miezi ya Shaabaniyya, Imamu Hussein, ndugu yake Abulfadhil Abbasi na Imamu Sajjaad (a.s).

Msaidizi wa mkuu wa chuo, Dokta Qaahirah Ulwaan amesema “Chuo kwa kushirikiana na idara ya maelekezo ya Dini katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa hafla kubwa ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Hussein, ndugu yake Abulfadhil Abbasi na Imamu Sajjaad (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Wanafunzi wa chuo walikuwa na nafasi kubwa katika utekelezaji wa ratiba ya hafla, sambamba na kutaja matukio muhimu katika historia za watukufu wanaoadhimishwa kuzaliwa kwao (a.s)”.

Idara ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake, imetoa muhadhara wa Dini uliojikita katika kuonyesha ushiriki wa wanawake katika kutangaza Dini, kuinusuru na kuilinda.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: