Idara ya Atabatu Abbasiyya imetembelea maeneo ya ukanda wa kijani.

Idara ya Atabatu Abbasiyya imetembelea maeneo ya ukanda wa kijani upande wa kusini mwa mkoa wa Karbala.

Idara hiyo imeongozwa na makamo katibu mkuu Mhandisi Abbasi Mussawi Ahmad, mjumbe wa kamati kuu Dokta Abbasi Didah Mussawi, mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Afdhalu Shami na baadhi ya masayyid na marais wa vitengo.

Rais wa kitengo cha ukanda wa kijani Sayyid Nasoro Hussein Mut’ibu amesema “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, kitengo kimetoa wito kwa waheshimiwa viongozi wa Ataba kuja kutembelea maeneo ya ukanda wa kijani, ili waone mazingira halisi na miradi muhimu inayoendelea katika eneo hili”.

Akaongeza kuwa “Ziara hii ni sehemu ya juhudi za Ataba tukufu katika kulinda mazingira na kuendeleza miradi ya kimkakati inayohusu utunzaji wa mazingira”.

Akaendelea kusema “Ujumbe huo umetembelea maeneo tofauti katika mradi wa kijani kibichi”, akasema “Hii ni hatua muhimu katika kuimarisha na kuendeleza utunzaji wa mazingira”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: