Idara ya Fatuma bint Asad ya masomo ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza majina ya washindi watatu wa shindano la (Waliozama katika elimu).
Shindano lilikua la kuhifadhi surat Alfat-hu na kutafakari aya zake kwa ushiriki wa kitaifa na kimataifa.
Zawadi zitatolewa siku ya Ijumaa ijayo kupitia ratiba ya “Ulizeni wanaojua” itakayofanywa ndani ya Sardabu ya Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) katika Ataba tukufu.
Iwapo mshindi atakaa mwezi mzima toka siku ya kutangazwa majina ya washindi, bila kuja kuchukua zawadi yake atakua amepoteza haki ya kupewa zawadi.
Shindano la (Waliozama katika elimu) linalenga kujenga jamii ya wanawake katika utamaduni wa kushikamana na mafundisho ya Dini na mwenendo wa Ahlulbait (a.s).