Kitengo cha Habari na utamaduni kimeshiriki kwenye kongamano la kielimu awamu ya saba la wahitimu wa shahada za juu.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimeshiriki kwenye kongamano la kielimu awamu ya saba la wahitimu wa shahada za juu.

Kongamano limefanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Qur’ani yetu utukufu wetu tutailinda kwa elimu yetu), limesimamiwa na uongozi wa idara ya malezi katika kitongoji cha Raswafah mjini Baghdad kwa kushirikiana na Atabatu Husseiniyya katika chuo kikuu cha Sibtwaini.

Ushiriki wa kitengo chetu kwenye maonyesho hayo unalenga kubadilishana uzowefu, maarifa na kuimarisha ushirikiano baina ya wanachuoni na watafiti, kwa lengo la kuboresha elimu na utamaduni wa Iraq.

Kongamano hilo linaonyesha jukudu kubwa inayofanywa ya kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi tofauti za kielimu za ndani na nje ya Iraq, sambamba na nafasi ya Atabatu Husseiniyya katika kusaidia tafiti za kielimu Pamoja na kuonyesha umuhimu wa elimu na ufahamu wa Qur’ani tukufu kwa kuzingatia maana zake katika Maisha ya kila siku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: