Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, kinatoa huduma kupitia tawi maalum linaloshiriki kwenye maonyesho ya Qur’ani katika chuo kikuu cha Kufa.
Kiongozi wa kituo bibi Sara Hafaar amesema “Kituo kimeshiriki kwenye maonyesho ya Qur’ani awamu ya pili yanayo simamiwa na Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya kwenye chuo kikuu cha Kufa kupitia tawi maalum, ikiwa ni Pamoja na kuonyesha machapisho mbalimbali yanayohusu jamii ya wanafunzi sambamba na kutoa ushauri wa kifamilia na kujibu maswali ya wanafunzi.
Akaongeza kuwa “Markazi ilianza kutoa huduma toka siku ya kwanza ya ufunguzi wa maonyesho hayo, na itaendelea hadi kesho siku ya Alkhamisi”, akasema kuwa “Tawi la kituo chetu limepata muitikio mkubwa kutoka kwa watu waliotutembelea”.