Kitengo cha Habari na utamaduni kimefanya nadwa kuhusu amani katika riwaya za Ahlulbait (a.s).

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya nadwa yenye anuani isemayo (Mazungumzo na athari yake katika kuleta amani kupitia riwaya za Ahlulbait -a.s-).

Kituo cha kuthibitisha jinai za magaidi kwa kushirikiana na kitivo cha Imamu Alkaadhim (a.s) cha elimu za kiislamu, kimeratibu nadwa siku ya Jumamosi ya tarehe (24/2/2024) saa kumi na moja jioni ndani ya ukumbi wa Imamu Murtadhwa (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya katika mkoa wa Najafu.

Nadwa hiyo ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kupambana na ukatili Pamoja na kusambaza ujumbe wa amani na kusameheana, sambamba na kufundisha uwelewa sahihi wa mafundisho ya Dini na utamaduni wa Ahlulbait (a.s) katika jamii ya Iraq na uislamu kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: