Ugeni wa makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya umbehudhuria maonyesho ya vitabu ya kimataifa awamu ya nne hapa Iraq.
Makamo rais wa kitengo cha makumbusho Dokta Shauqi Mussawi amesema, “Maonyesho yanasimamiwa na taasisi ya Habari na utamaduni chini ya kauli mbiu isemayo (Ikawa inaitwa Palestina), kwa ushiriki wa zaidi ya taasisi za usambajaji (350) kutoka ndani na nje ya Iraq, jumla ya nchi (16) zinashiriki kwenye maonyesho hayo”.
Akaongeza kuwa “Kitengo cha makumbusho kimeshiriki kwenye maonyesho hayo kwa ajili ya kunufaika na machapisho mbalimbali kuhusu makumbusho na masomo ya kiislamu kwa lugha ya kiarabu na lugha za kigeni, sambamba na kulinganisha na mali-kale zilizopo kwenye makumbusho ya Alkafeel”.
Akaendelea kusema “Maktaba itachangia katika kusaidia watafiti kuwapatia vitabu muhimu na adumu, Pamoja na kusaidia harakati za kitamaduni, kwa hiyo tumeongeza juhudi ya kuweka vitabu mbalimbali ili kuifanywa kuwa marejeo muhimu kwa watafiti”.
Makumbusho ya Alkafeel inaendelea kutembelea maonyesho ya vitabu na makumbusho kwenye miji tofauti, kwa lengo la kuangalia machapisho mapya yanayohusu turathi na elimu zingine.