Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya semina ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa Dini wenye asili ya Afrika wanaoishi hapa Iraq.
Kiongozi wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema “Markazi imefanya semina ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa Dini wenye asili ya Afrika wanaoishi Iraq”, akasema “Semina hii ni sehemu ya mkakati wa kuwajengea uwezo wa kitablighi washiriki, na kuwafundisha njia rahisi za kufikisha ujumbe kwa walengwa”.
Akaongeza kuwa “Mkufunzi wa semina alikuwa ni Dokta Mustwafa Ibrahimi, ameeleza njia za kisasa katika Tablighi na namna ya kuwasiliana na umma kwa kufikia lengo la kufikisha ujumbe kusudiwa”.
Akaendelea kusema “Wanafunzi walioshiriki kwenye semina wametoka nchi tofauti za Afrika, amabzo ni Naijeria, Brokinafaso, Kenya, Averikosti na Ethiopia”.
Wanafunzi wameshukuru Markazi Dirasaati Afriqiyya kwa kuwajengea uwezo wa kitabligh, na kuwaandaa vizuri ili wawezo kutekeleza jukumu lao kwa mafanikio katika bara la Afrika.