Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inafanya mradi wa Qur’ani wa (Nyumba za Nuru) katika mkoa wa Karbala.
Mradi huo unatekelezwa katika nyumba za waumini chini ya kauli mbiu isemayo (Mfano wa familia inayotazama kwa Qur’ani), na usimamizi wa idara ya harakati za Qur’ani katika Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa.
Kiongozi wa idara Dokta Ali Hamdi Kakawi amesema “Vikao vya usomaji wa Qur’ani hufanywa katika misikiti na husseiniyya, hivi sasa tumeteua baadhi ya nyumba ambazo familia zake zitaneemeka kwa kusikiliza kitabu cha Mwenyezi Mungu na kuwaongezea Imani, Uchamungu na mapenzi ya Qur’ani tukufu”.
Atabatu Abbasiyya kupitia vitengo vyake, inafanya kila iwezalo kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii, kwa kuendesha visomo vya Qur’ani kwenye misikiti, shule na majumbani.