Makumbusho ya Alkafeel imejadiliana na makumbusho ya Atabatu Husseiniyya njia za kuimarisha ushirikiano baina yao.

Ujumbe kutoka makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya umejadiliana na viongozi wa makumbusho ya Atabatu Husseiniyya njia za kushirikiana katika sekta ya utunzaji wa mali-kale na namna ya uwekwaji wake katika makumbusho.

Yamesemwa hayo kupitia ziara ya ujumbe ulioongozwa na mkuu wa kitengo cha makumbusho Sayyid Swadiq Laazim Zaidi na msaidizi wake Dokta Shauqi Mussawi wakiwa na baadhi ya watumishi katika makumbusho ya Imamu Hussein (a.s) iliyochini ya Atabatu Husseiniyya.

Zaidi akasema kuwa, “Kutokana na mnasaba wa kuadhimisha mazazi ya Maimamu watakatifu (a.s) chini ya mpango wa kutembelea makumbusho za Ataba, ujumbe wetu umetembelea makumbusho ya Imamu Hussein (a.s) iliyochini ya Atabatu Husseiniyya kwa lengo la kujadili njia za kushirikiana baina ya pande mbili”.

Akaongeza kuwa “Ataba mbili tukufu zinaandaa majengo mapya, kuna haja kubwa ya kukutana na kubadilishana mawazo kuhusu utunzaji wa mali-kale sambamba na kuchagua zinazofaa kuwekwa kwenye makumbusho”.

Kiongozi wa makumbusho ya Imamu Hussein (a.s) Sayyid Ghasaan Shahristani amesema “Ujumbe wa makumbusho ya Alkafeel umetuzawadia jiwe (mali-kale) kutoka kwenye kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kutambulishwa kwa ufupi kuhusu mali-kale zilizopo katika makumbusho ya Atabatu Husseiniyya na harakati zinazofanywa na kamumbusho hii tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: