Idara ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa huduma za kuelekeza mazuwaru wa mwezi kumi na tano Shabani sambamba na kuadhimisha mazazi ya Imamu Mahadi (a.s).
Kiongozi wa idara ya kujibu maswali kisheria bibi Zaharaa Jaasim amesema, “Nafasi ya waelekezaji ni kusahihisha mambo ya kisheria na kujibu maswali ya mazuwaru watukufu kwa njia ya papo hapo, simu au mitandao ya kijamii”.
Akaongeza kuwa “Idara hupokea idadi kubwa ya mazuwaru kutoka mataifa tofauti kila siku, na huwapa majibu ya kisheria kutokana na maswali yao, pamoja na kuwafafanulia ulazima wa kushikamana na sheria wakati wote na hususan wanapokua katika ziara tukufu”.
Idara ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake hutumia matukio kama haya kutoa mafundisho mbalimbali kwa mazuwaru ili kuwafanya wawe mfano mwema wa kuigwa.