Kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya kinafanya kazi kubwa ya kuratibu matembezi ya mazuwaru wanaokuja kuhuisha mazazi ya Imamu Mahadi (a.f).
Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Zainul-Aabidina Quraishi amesema “Watumishi wa kitengo wanafanya kazi kubwa ya kuhudumia mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wa ziara ya Shaabaniyya, miongoni mwa huduma wanazotoa ni kuongoza matembezi ya mazuwaru wakati wa kuingia na kutoka ndani ya haram tukufu pamoja na kuandaa sehemu maalum za kufanyia ibada”.
Akaongeza kuwa “Walianza kusafisha sehemu zote ndani ya haram tukufu, kupuliza marashi, kuweka vitabu vya ziara, turba sambamba na kugawa pipi (halwa) katika kuadhimisha mazazi ya Imamu msubiriwa (a.f)”.
Kitengo cha kusimamia haram tukufu kinamajukumu mengi ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama vile kupiga deki, kusafisha na kutandika miswala.