Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinatoa huduma za kitablighi kwa mazuwaru wa mwezi kumi na tano Shabani kupitia vituo (15).
Rais wa kitengo Shekhe Swalahu Karbalai amesema “Kitengo kimeanza kutekeleza ratiba ya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani kupitia vituo (15) tofauti vilivyo funguliwa katika mji na Barabara zinazo elekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na eneo linalozunguka malalo takatifu, bila kusahau vituo vilivyo funguliwa karibu na Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f)”.
Akaongeza kuwa “Kitengo kimetumia baadhi ya Mashekhe wanaojua lugha za kigeni kwa ajili ya kujibu maswali ya mazuwaru wanaokuja kutoka nchi zisizokua za kiarabu”.
Kitengo kimeweka majukwaa yanayotumika kutolewa maelekezo mbalimbali kwa mazuwaru pamoja na kusoma usia maalum wa Marjaa-Dini mkuu Sayyid Ali Sistani katika ziara hii.