Kitengo cha afya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kutoa huduma kwa zaidi ya matukio (300,000) wakati wa ziara ya Shaabaniyya.
Rais wa kitengo hicho Dokta Haifaa Tamimi amesema “Kitengo kilikua na vituo saba vya kutolea huduma za afya katika maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu na kwenye Barabara zinazoelekea Ataba, vituo vinne vya wanawake, vimehudumia matukio (106,029), vituo vitatu vya wanaume vimehudumia matukio (119,272), hivyo jumla ya wanufaika ni (225,301)”.
Akaongeza kuwa “Idadi ya wagonjwa waliopewa matibabu ya moja kwa moja ilifika (116,715), hivyo idadi jumla ya wanufaika inakua (342,016) akasema, hakukuwa na tukio lolote la hatari au kifo kwa mazuwaru”.
Akasisitiza kuwa “Kitengo kinaendelea kutoa huduma za afya kwa mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wote na kwenye matukio yote makubwa”.