Kitengo cha makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimesema kuwa makundi ya mazuwaru yameingia katika makumbusho hiyo ndani ya Ataba tukufu, wakati wa ziara ya Shaabaniyya.
Kiongozi wa idara ya ukumbi wa maonyesho Sayyid Mahmuud Muhammad Murtadhwa amesema “Idadi kubwa ya mazuwaru wa mwezi kumi na tano Shabani, wameingia katika ukumbi wa makumbusho ndani ya Atabatu Abbasiyya”.
Akaongeza kuwa “Ukumbi unaidadi kubwa ya mali-kale muhimu na adimu zinazohusu historia ya Atabatu Abbasiyya tukufu” akasema “Milango ya ukumbi wa makumbusho ilikua wazi hadi usiku wakati wa ziara ya Shaabaniyya”.
Mji wa Karbala umepokea maelfu ya watu waliokuja kutoa pongezi za kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f) katika malalo mbili tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).