Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimezundua mtandao wa kupakua App ya Haqibatu Mu-Umin kupitia jukwaa la Whatssap.
Mkuu wa kituo cha mitandao na program za kiislamu Sayyid Ali Jayashi amesema “Kituo kimezindua mtandao wa kupakua App ya Haqibatu Mu-Umin kutipia Whatssap, imepata muitikio mkubwa sana katika siku za mwanzo, imepata zaidi ya washiriki (elfu 35) thelathini na tano elfu”.
Akaongeza kuwa “Kuzindua mtandao wa kupakua App hiyo kupitia Whatssap, ni sehemu ya kutekeleza jukumu la kufundisha elimu ya Mtume Muhammad na watu wa nyumbani kwake (a.s) kupitia majukwaa ya mitandao tofauti ya kijamii, App hiyo inamasomo ya Dini, ibada za kila siku, Qur’ani tukufu, Ziara, Dua na matukio mengine”.