Shule za Alkafeel za wasichana zimekamilisha kutengeneza vyeti vya washiriki wa hafla kuhitimu kwa mabinti wa Alkafeel awamu ya saba.

Watumishi wa idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya, wamekamilisha uchapishaji wa vyeti vya washiriki wa hafla ya wahitimu wa Alkafeel awamu ya saba.

Hafla itafanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Ulimwengu unan’gaa kutokana na nuru ya Fatuma), washiriki watakuwa (3000) kutoka mikoa (15).

Kiongozi wa idara bibi Bushra Kinani amesema “Uchapishaji wa vyeti vya wanafunzi wa vyuo watakao shiriki kwenye hafla ni sehemu ya majukumu yetu”.

Akaongeza kuwa “Vyeti vimetengenezwa rasmi kwa ajili ya wahitimu wa mahafali hii chini ya utaratibu uliowekwa na idara”.

Atabatu Abbasiyya hufanya hafla za wahitimu kila mwaka, toka kuanza kwa utaratibu huo huu ni mwaka wa saba, hafla itafanywa siku ya Ijumaa sawa na tarehe (1/3/2024m), itakuwa na vipengele tofauti, vinavyo wajenga wanafunzi na wahitimu, safari yao ya masomo wanaihitimisha na kuanza safari ya kazi wakiwa ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: