Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeendesha ratiba ya msimu wa Qur’ani ya Mahdawiyyu kwenye chule, vyuo na maahadi katika mkoa wa Dhiqaar.
Ratiba hiyo imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mkoa wa Dhiqaar chini ya Majmaa.
Kiongozi wa Maahadi Sayyid Ali Albayati amesema “Msimu wa Mahdawiyyu ni sehemu ya ratiba ya (Amana iliyotunzwa) inayosimamiwa na Majmaa-Ilmi kupitia Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Dhiqaar, kwa lengo la kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s) kwa ujumla, likiwemo la kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f) katika msimu huu”.
Akaongeza kuwa “Sehemu ya kwanza ya ratiba hiyo imejikita katika kufanya vikao vya usomaji wa Qur’ani na mashindano ya kielimu katika shule na vyuo vya mkoa wa Dhiqaar”.
Ratiba itadumu kuanzia tarehe (16 – 30) Shabani 1445h, sawa na (27 – 11) Machi 2024m kwa kushirikiana na uongozi wa malezi, vyuo na Maahadi za hapa mkoani.