Kuadhimisha mazazi yake matukufu.. kituo cha utamaduni wa familia kimetoa muhadhara kuhusu Imamu Mahadi (a.f).

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kimetoa muhadhara kuhusu Imamu Mahadi (a.f) katika kuadhimisha mazazi yake.

Mkuu wa kituo bibi Sara Alhafaar amesema “Kituo kimetoa muhadhara wa kitamaduni wenye anuani isemayo (Katika zama za giza: Tafakari kuhusu Imamu Mahadi (a.f) na mategemeo ya kesho bora) katika maadhimisho ya mazazi matukufu mwezi kumi na tano Shabani”.

Akaongeza kuwa “Muhadhara umetolewa na mbobezi wa mambo ya kisaikolojia na urekebishaji wa maadili Dokta Shaimaa Nasoro, amefafanua sifa za mtu anayesubiri na namna ya kumtegemea Mwenyezi Mungu mtukufu, mada ilijikita katika kueleza nafasi ya wanaosubiri”.

Akaendelea kusema “Baada ya muhadhara, idara ya kituo ikatoa zawadi kwa washindi wa shindano la (muokozi wa umma) lililosimamiwa na kituo kwa njia ya mtandao”.

Kituo kinaendelea kutumia matukio ya Ahlulbait (a.s) katika kufundisha utamaduni wao kidini na kimalezi kwa lengo la kulinda misingi ya uislamu katika jamii ya wanawake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: