Uzinduzi huo umefanywa kwenye nadwa ya kielimu iliyosimamiwa ma kituo cha kuhuisha turathi, chini ya kamati kuu ya kuhuisha turathi katika Ataba tukufu, iitwayo (Shekhe Hussein Abduswamad Al-Aamiliy -mzazi wa Shekhe Bahaaiy).
Kitabu kina juzuu mbili zenye anuani ya kujitegemea na juzuu tatu zenye jumbe 15 za kifiqhi.
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya amepongeza nadwa iliyosimamiwa na kituo cha kuhuisha turathi, chini ya kamati kuu ya kuhuisha turathi katika Ataba tukufu.
Sayyid Swafi ametoa maoni yake baada ya mada iliyotolewa na mkuu wa taasisi ya turathi za kishia nchini Iran Shekhe Ridhwa Mukhtari, iliyokua na anuani isemayo (Uhusiano wa Shekhe Hussein bun Abduswamad Al-Aamiliy mzazi wa Shekhe Bahaaiy na shahidi wa pili), hakika shahidi wa pili (Zainu-Dini bun Ali Ji’iy Al-Aamiliy) alikua faqihi mkubwa mwenye rai nyingi, aliakisi mzazi wa Shekhe Bahaaiy, anaesoma turathi za Shekhe Hussein bun Abduswamad Bahaaiy atadhani ni miongoni mwa fikra zake, wakati sio hivyo ni miongoni mwa matunda ya Shahidi wa pili, lakini utoaji wa mas-ala ya kifiqhi muhimu kwa historia, kwa sababu ni sehemu muhimu kwa turathi zetu za kifiqhi, mtoa mada amesema asili ya mas-alah ya (Istiswhaab) inanasibishwa na Mzazi wa Shekhe Bahaaiy”.
Akaongeza kuwa “Baadhi ya maoni yanaweza kutokea kati ya mwanafunzi na mwalimu wake, halafu mwanafunzi akayaboresha hata kama mwalimu hatoyajata maoni hayo katika vitavu vyake, uhusiano wa mwalimu na mwanafunzi unahitaji kutambua sekta ya elimu, ndio kitu tunachohitaji katika kutambua rai za Shekhe Hussein Al-Aamiliy kwa Shahidi wa pili”.
Nadwa imejadili tafiti tofauti katika Maisha ya Shekhe Hussein bun Abduswamad Al-Aamiliy na turathi zake za kifiqhi.