Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amewapa zawadi watafiti walioshiriki kutoa mada kwenye nadwa ya kielimu ya kuhuisha turathi.
Kituo cha kuhuisha turathi chini ya kamati ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya nadwa ya kielimu kuhusu Shekhe Hussein Abduswamad Al-Aamiliy mzazi wa Shekhe Bahaaiy, imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, baadhi wa wajumbe wa kamati kuu na viongozi wa kisekula na kihauza.
Waliopewa zawadi ni (Shekhe Ridhwa Mukhtari, Shekhe Muhammad Taqi Faqiih, Shekhe Amiir Ridhwa Nishaburi, Muhammad Kaadhim Rahmati na Shekhe Liith Karbalai), pamoja na muendesha kikao cha uwasilishaji wa tafiti hizo Dokta Ali Khadhwiri.
Katika nadwa hiyo umefanyika uzinduzi wa kitabu cha turathi za kifiqhi cha mzazi wa Shekhe Bahaaiy (Shekhe Hussein bun Abduswamad Haarithi Al-Aamiliy) na muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, sambamba na kujadili tafiti mbalimbali kuhusu turathi za kifiqhi.