Asubuhi ya Ijumaa ratiba ya siku ya pili ya mahafali ya wahitimu kikosi cha mabinti wa Alkafeel awamu ya saba yenye washiriki (3000) kutoka vyuo vikuu tofauti vya Iraq ilianza.
Mahafali imeratibiwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Ataba tukufu, inafanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Ulimwengu unaangazwa kutokana na nuru ya Fatuma -a.s-), washiriki wanatoka katika mikoa (15).
Mahafali imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyosomwa na Sayyid Haidari Jalukhani, na muongoza mahafami (mc) alikua ni Sayyid Yusufu Twaaiy, ikafuatiwa na kusoma kiapo cha kuhitimu na utii wa kulitumikia taifa mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika uwanja wa mlango wa Qibla.
Mahafali ya mabinti wa Alkafeel awamu ya saba ni miongoni mwa mahafali kubwa inayofanywa na Atabatu Abbasiyya kwa wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq, wahitimu hula kiapo cha kuanza Maisha ya kazi mbele ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).











































