Sayyid Swafi amekhutubia wanafunzi elfu tatu kutoka mikoa (15) ya Iraq, wenye Dini na madhehebu tofauti, ujumbe wa hutuba yake unasema:
- 1- Hakika tunajivuna na kuonyesha mfano huu mwema mbele ya dunia, hakika hawa ndio mabinti wa Iraq waliozaliwa na wakinamama watukufu.
- 2- Tunapo angalia mahafali hii, tunaiona idadi kubwa katika jamii imeshiriki pamoja na nyie katika furaha yenu.
- 3- Enyi mabinti watukufu, wazuri, mnaojistiri, wapole, sasahivi mnaishara nyingi za uchamungu, Imani, nguvu, usafi, Maisha mema, yote hayo ni fahari kwetu.
- 4- Nyie ni matunda mazuri ya shule na mmesoma kiapo cha ahadi ya kuhitimu, mtatekeleza kila jambo jema kwa ufanisi mkubwa.
- 5- Ewe mwanafunzi wewe ni imara unauwezo wa kubadilisha jamii nzima, wewe ni mbegu ya kujenga jamii na familia.
- 6- Kuna vita ya kumuondoa mwanamke katika misingi ya Maisha bora, na mwanamke ndio Maisha.
- 7- Nyie ndio tegemeo la kutengeneza tabasamu katika familia, mnatakiwa mrejeshe fadhila ya kazi kubwa iliyofanywa na familia zenu.
- 8- Sisi tunapenda kuwaona katika hali nzuri daima, ambayo mzazi hupenda kumuona mwanae, baba anapenda kuwaona wanae wakiwa katika hali bora kumshinda na mama anapenda kumuona binti wake akiwa bora zaidi yake.
- 9- Tunapoangalia mabinti zetu katika muonekano huu mzuri wa kiroho na haiba hii, tunafurahi.
- 10- Iraq ni nchi ya elimu, maadili na ubinaadamu, nyie ni sehemu ya watatuzi wa changamoto zake, tunaamini changamoto zote zitatatuliwa na nyie.
- 11- Huu mkono umesimama mbele ya kaburi la mbora wa kujitolea na uaminifu, kamanda miongoni mwa makamanda wa Karbala, mkono huu hautakiwi kunyooshwa kwa mtu muovu.
- 12- Natoa shukrani nyingi kwa vyuo vikuu na walimu watukufu kwa kazi kubwa na nzuri ya kufundisha elim na maadili kwa vijana na mabinti zetu.