Majmaa-Ilmi imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika mji wa Baghdad.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika kukumbuka watakatifu waliozaliwa ndani ya mwezi wa Shabani.

Hafla hiyo imefanywa katika wilata ya Husseiniyya jijini Baghad chini ya usimamizi wa Maahadi ya Qur’ani tawi la Baghdad.

Wasomaji waliodhiriki katika hafla hiyo ni, Abu Yusufu Mahmadawi, msomaji wa Atabatu Kaadhimiyya Dokta Raafii Al-Aamiriy, Muhammad Baaqir Alhamdani, aidha kulikua na usomaji wa tenzi na qaswida kutoka kwa Maahadi Ali Dhahabi, hafla ikahitimishwa kwa usomaji wa dua ya Faraj.

Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyake, inafanya kila iwezalo katika kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani kwa makundi tofauti ya jamii, kwa kufanya vikao vya usomaji wa Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: