Kiongozi wa kituo Sayyid Ali Hassan Bahadeli amesema “Kituo cha Ummul-Banina (a.s) cha tiba ya meno, kimepokea mayatima (25) kutoka mkoa wa Misaan, na kuwapa huduma tofauti za matibabu ya meno chini ya kikosi-kazi cha madaktari waliochini ya kituo”.
Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imegharamia kila kitu, kuanzia usafiri, makazi na chakula, ratiba hii ilianzishwa na kiongozi mkuuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi toka mwaka 2013m, bado inaendelea hadi leo”.
Akasema kuwa “Toka kuanza kwa ratiba hii hadi leo idadi ya wanufaika ni zaidi ya watoto elfu (15) kutoka mikoa tofauti ya Iraq”.