Msimamizi wa tawi la Alkafeel Sayyid Ridhwa Swafi amesema: Ushiriki wa kituo cha Alkafeel chini ya chuo kikuu cha Alkafeel kwenye kongamano la (Ainul-Hayaa) la pili, umejikita katika mambo manne ya kimtandao.
Akaongeza kuwa: Kulikua na mfumo wa tiba wa idara za taasisi za afya, mfumo wa siraaji kwa idara za vyuo, jukwaa la siraji la masomo, na mfumo wa Aljuud.
Kwa mujibu wa Swafi, lengo la kushiriki kwenye kongamano hili ni kutambulisha mifumo ya kimtandao na kuonyesha mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta hiyo, na umuhimu wa huduma zinazotolewa kwa mtu mmoja mmoja na jamii.