Chuo kikuu cha Al-Ameed kimeshiriki kwenye kongamano la (Ainul-Hayaa) linalofanywa jijini Baghdad kikiwa na mifumo minne ya kielektronik.
Waratibu wa kongamano hilo ni taasisi ya kitamaduni na kimaendeleo Alqabsu kwa ushiriki wa Ataba tukufu.
Muwakilishi wa tawi Dokta Buriri Al-Atwaar amesema “Ushiriki wa chuo kwenye kongamano la (Ainul-Hayaa) umehusisha kitengo cha kompyuta na mitandao, kwa kuonyesha mifumo minne ya mitandao ambayo ni (Mfumo wa mitandao ya kielektronik, mfumo wa kutuma maombi na maelezo yake, mfumo wa mambo ya kibinaadamu, na toghuti rasmi ya chuo)”.
Akaongeza kuwa “Miradi imeanzishwa na raia wa Iraq ndani ya chuo, kwa lengo la kuwapa wanafunzi kitu kilicho bora zaidi na kwa faida ya wote”.
Ushiriki wa chuo kikuu cha Al-Ameed ni sehemu ya kupanua wigo wa utaalamu wa kimitandao na kubadilishana uzowefu baina ya vyuo vikuu.