Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimehitimisha ratiba ya (Juu ya muongozo wako ewe kiongozi wangu) awamu ya tano jijini Baghdad.
Kiongozi wa kituo bibi Sara Alhafaar amesema “Kituo cha utamaduni wa familia kimehitimisha ratiba ya (Juu ya muongozo wako ewe kiongozi wangu) awamu ya tano katika mkoa wa Baghdad”.
Akaongeza kuwa “Ratiba ya leo imepambwa na muhadhara wenye anuani isemayo (Nanma ya kujiepusha na changamoto za kinafsi), umetolewa na mbobezi wa mambo ya kisaikolojia na urekebishaji wa maadili Dokta Shaimaa Nasoro, ameongea kuhusu changamoto za kimaadili, sababu zake na njia za kuzitatua”.
Akaendelea kusema “Muhadhara umeeleza namna bora ya kuboresha maadili na kujielekeza katika kufanya mambo mema yanayomridhisha Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s)”.