Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kinatoa mafunzo ya utumiaji wa kompyuta kwa baadhi ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Mkufunzi wa semina hiyo Sayyid Mustwafa Alhakiim amesema, “Semina inalenga kufundisha mambo ya msingi katika kutumia kompyuta”.
Akaongeza kuwa “Wamefundishwa mada tofauti, miongoni mwa mada hizo ni, historia ya kuanzishwa kwa komyuta na aina zake, kutambua mifumo endeshi ya kompyuta, namna ya kutumia mifumo ya window, namna bora ya kutunza faili au taarifa na njia ya kutatua baadhi ya matatizo ya program”.
Akaendelea kusema kuwa “Semina inafanywa ndani ya ukumbi wa Naafidhu-Albaswirah na itadumu kwa siku tatu (3), kila siku watasoma kwa muda wa saa nne (4)”.