Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, kimeanza kukarabati misikiti ya vyuoni.
Kazi hiyo inafanywa na idara ya vyuo vikuu na shule chini ya kitengo.
Wamejikita katika kukarabati misikiti ya vyuo na taasisi za elimu ya juu, wameanza kwa kukarabati misikiti miwili katika chuo cha Dujlah jijini Baghdad na misikiti miwili katika chuo cha Kirkuuk.
Misikiti inawekwa kila kitu cha lazima, kazi hiyo inaimarisha uhusiano na jamii ya wanafunzi.
Atabatu Abbasiyya tukufu inajenga mazingira bora ya kiimani na kiibada kwa wanafunzi kuputua mradi huo.