Hafla itafanywa jioni ya Ijumaa (8/3/2024) chini ya kauli mbiu isemayo (Hijabu yangu ni msingi wa stara na usafi wanyu), jumla ya wanafunzi (770) wa shule za Al-Ameed wamefikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria na watashiriki kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa shule za Al-Ameed za wasichana bibi Mina Waaili amesema “Watumishi wa shule za Al-Ameed wamekamilisha mafunzo maalum kulingana na mahitaji ya ushiriki wa hafla ya kuwajibikiwa na sheria itakayo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Akaongeza kuwa “Uingiaji wa wanafunzi na kusimama kwenye jukwaa kuu utakua kwa utaratibu maalum, wataingia kwa mistari iliyopangika kwa umaridadi wa hali ya juu”.
Halfa inalenga kuwajulisha wanafunzi kuhusu hatua waliyofikia katika umri wao na umuhimi wa kutekeleza mafundisho ya Dini na kushiriki kazi za kijamii sambamba na kuwafundisha mwenendo sahihi katika maisha yao kidini na kijamii.