Maqaam tukufu ya Imamu Hujjat (a.f), asubuhi ya kila siku ya Ijumaa hushuhudia kundi kubwa la waumini wanaokuja kusoma Dua-Nudba.
Dua husomwa katika mazingira tulivu ya kiibada kwa baraka za mnasibishwa wa Dua hiyo sambamba na ushiriki wa idadi kubwa ya mazuwaru.
Watumishi wa Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) hufanya kila wawezalo katika kuandaa mazingira mazuri ya kiibada, huweka vitabu vya dua vya kutosha, huandaa sehemu maalum za ibada, hupuliza marashi, husimamia ukaaji wa watu kwa kuwapanga vizuri na huandaa muongozaji wa kusoma dua pamoja na huduma zingine.