Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya shindano la kusoma Qur’ani kwa kuhifadhi na kuangalia kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Karbala.
Shindano limeratibiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa, kwa kushirikiana na kitivo cha uuguzi hapo chuoni.
Shindano limepambwa na ujumbe kutoka kwa msaidizi wa mkuu wa kitivo cha uuguzi Dokta Hassan Abdallah, ameishukuru Ataba kwa msaada endelevu wa kufundisha Dini katika jamii.
Shindano lilikua na ushindani mkali, limeongozwa na kamati mahiri yenye wajumbe wafuatao, Dokta Muhammad Twayaar, Dokta Ali Hamdi Kalkawi, Ustadh Hussein Alkhafaji na Mustwafa Saadun.
Mwanafunzi Amiri Qahtwani ameibuka mshindi wa kwanza kwenye shindano hilo, amepewa zawadi maalum na mkuu wa chuo, sambamba na kutoa zawadi kwa washiriki wote na kamati ya majaji.