Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya imewazawadia walimu (2120) kutoka shule (63) za mkoa wa Karbala katika siku ya mwalimu.
Kiongozi mkuu wa jumuiya Ali Hussein Abduzaid amesema “Zawadi hizo zinaonyesha nafasi kubwa aliyonayo mwalimu katika kujenga jamii, hakika walimu wanakazi kubwa ya kufundisha na kuelekeza wanafunzi katika njia sahihi”.
Akaongeza kuwa “Hafla ya ugawaji wa zawadi ilikua na vipengele tofauti, kulikuwa na uwasilishaji wa pongezi, usomaji wa tenzi na mashairi, mada kuhusu nafasi ya mwalimu katika malezi, kisha walimu (2120) wakapewa zawadi”.
Akaendelea kusema “Jumuiya imetoa shukrani kwa wazazi wa vijana wa Skaut, ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha shughuli hii muhimu”.