Ameyasema hayo alipopokea idara ya jumuiya ya kutunza watoto wenye maradhi ya kisukari katika mji wa Baabil pamoja na watoto wenye maradhi hayo, ambapo amesikiliza maelezo kuhusu utendaji wa jumuiya hiyo na juhudi zake katika kuhudumia na kutibu watoto wenye kisukari na changamoto walizonazo.
Sayyid Swafi amepongeza mradi huo wa kibinaadamu na kazi nzuri inayofanywa na idara ya taasisi, akawatakia mafanikio mema, akabainisha kuwa maradhi ya sukari yameenea kwa watoto na wakubwa.
Akasisitiza ulazima wa kushiriki kupambana na maradhi hayo kila mmoja kwa namna anavyo weza, Daktari anaweza kubaini maradhi na kutoa tiba, kuna mtu mwenye uwezo wa kupunguza makali ya maradhi, mwingine anaweza kuhudumia wagonjwa, hakika hakuna jambo bora zaidi ya kuhudumia watu, na kuhudumia watoto hawa ni jambo tukufu zaidi.
Sayyid Swafi ametoa wito kwa mamlaka zinazo husika kuweka mazingira mazuri kwa jumuiya hiyo, akathibitisha kuwa Atabatu Abbasiyya itasaidia juhudi za jumuiya, ameahidi kuwapa nafasi za masomo katika shule za Ataba watoto wenye alama za juu miongoni mwao, sambamba na kuwapa gari kwa ajili ya shughuli za jumuiya kama walivyo omba aidha maombi yao yote yamezingatiwa.
Atabatu Abbasiyya imesha wahi kuwapa baadhi ya mahitaji ya lazima kwa wagonjwa wa kisukari, huo ulikua msaada wa kwanza mkubwa hapa Iraq, kwa mujibu wa kiongozi wa jumuiya ya kulea watoto wenye maradhi ya sukari katika mkoa wa Baabil bibi Lina Shimri.