Ameyasema hayo alipompokea mkuu wa kitivo cha elimu ya kiislamu kutoka chuo kikuu cha Baabil Dokta Hassan Ubaidi Maamuri na wenzake, akasikiliza maelezo kuhusu kitivo hicho na mahitaji yake kulingana na changamoto zilizopo.
Sayyid Swafi katika mazungumzo yake amesisitiza umuhimu wa kufikisha elimu kwa mwanafunzi kwa kutumia njia sahihi inayofaa.
Muheshimiwa akabainisha kuwa, Mwalimu anapokua na maarifa mengi yanamsadia kutumia njia salama katika ufikishaji wa elimu kwa wanafunzi.
Akahimiza umuhimu wa kuchukua masomo ya juu kutoka kwenye tafiti za wanachuoni wakubwa, akafafanua kuwa umma wa kiislamu na Iraq kwa ujumla ni tajiri wa wanachuoni.
Sayyid Swafi ameiambia kamati ya viongozi wa Ataba tukufu iende kuangalia hali halisi ya kitivo hicho na kusaidia baadhi ya mahitaji ya kielimu, watumie uzowefu walionao kutoka vyuo vingine kikiwemo chuo kikuu cha Baabil.
Maamuri amesema kuwa “Mazungumzo yalijikita katika harakati za Qur’ani, maarifa ya Dini na kusikiliza nasaha kutoka kwa muheshimiwa kuhusu harakati na athari yake katika jamii upande wa kufanyia kazi Qur’ani tukufu na uwelewa wa Ahlulbait (a.s) katika malezi ya vijana”.
Akaongeza kuwa “Tumeongea kuhusu ushirikiano endelevu na Atabatu Abbasiyya katika kufanya makongamano yanayosaidia kuinua kiwango cha elimu kwa vijana”.