Kitengo cha habari na utamaduni kinatoa huduma ya kibinaadamu katika mwezi wa Ramadhani kwa waafrika wanaoishi Iraq.

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa huduma ya kibinaadamu kwa waafrika wanaoishi Iraq.

Huduma hiyo inatokana na kuingia kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, nayo ni sehemu ya mradi wa kapu la chakula unaolenga kugawa chakula kwa raia wenye asili ya Afrika wanaoishi Iraq.

Ugawaji wa furushi la chakula umelenga waafrika wanaoishi katika mji wa Najafu na Karbala.

Familia za waafrika waliopewa chakula, wameishukuru Markazi na kupongeza kazi kubwa zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kusaidia jamii za waafrika kwenye nchi tofauti za Afrika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: