Ameyasema hayo wakati akiongea na wasimamizi ya mradi wa kujenga uwezo wa watumishi wa Ataba tukufu, unayoendeshwa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, baada ya kusikiliza maelezo ya viongozi hao na baadhi ya wanufaika wa ratiba hiyo katika mwaka 2023.
Sayyid Swafi akasema, Kila mtu anaependa kuanzisha jambo zuri linye manufaa, akapata changamoto na lazima atumie muda kupambana na changamoto hizo.
Akabainisha kuwa, mtu anapotaka mafanikio lazima awe na maono ya wazi anayoweza kuyaonyesha kwa vitendo mbele ya wanufaika.
Akasisitiza kuwa, watumishi wa Ataba tukufu wanahitaji kuongeza maarifa na kutambua miradi ya Ataba.
Akaendelea kusema, wasimamizi wa ratiba hiyo lazima waweze kuathiri mwenendo wa mtumishi na kumfanya kuwa mtumishi bora wa kupigiwa mfano, hii ndio sifa kubwa waliyonayo watumishi wa Atabatu Abbasiyya kwa sasa, ni wazi kuwa wanaheshimu mazuwaru na kuwafanyia kila jambo zuri wanaloweza kufanya sambamba na kuheshimu taratibu na kanuni za ndani na nje ya Ataba.
Akasisitiza umuhimu wa kutoa nasaha kwa watumishi na kuwapa muongozo Pamoja na kuwatambulisha haki na wajibu wao, na kuweka uhusiano mzuri kati ya mtumishi na rais wa kitengo katika misingi ya kuheshimiana na kulinda mipaka ya kiidara.
Rais wa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu Dokta Muhammad Hassan Jabiri amesema, Shughuli zinazofanywa na vitengo tofauti vya Ataba, zinatokana na msisitizo wa kiongozi mkuu wa kisheria Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, katika mwaka uliopita idadi ya wanufaika wa mradi huo ilifika watumishi (3000).
Akaongeza kuwa, kamati ya viongozi ikaeleza mafanikio yao na ikasikiliza maelekezo ya Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria yaliyo onyesha hamu ya kuwa na watumishi bora wa kupigiwa mfano.